Ligi Kuu

Kocha aota mbawa, Yanga yaamua kuanza upya

Sambaza....

Alietarajiwa kuwa kocha Mkuu wa Yanga raia wa Burundi Cedrick Kaze ameshindwa kujiunga na timu ya Wananchi kutokana na sababu zilizo zilizotajwa na klabu ya Yanga.

Kwa mujibu wa taarifa rasmi ya klabu imesema kocha huyo ameomba kupewa wiki tatu zaidi ndipo ajiunge na Yanga kutokana na sababu za kifamilia na klabu ya Yanga imeona hawana muda wa kumsubiria yeye.

Kitendo hicho kimewafanya Yanga kuachana na kocha huyo na kuamua kurudi tena katika maombi ya mwanzo na kuanza kutafuta kocha mpya haraka iwezekanavyo. Tazama barua rasmi ya klabu

Kwa maana hiyo Yanga bado itaendelea kuwa chini ya mwalimu wa viungo Rido raia wa Afrika Kusini huku pia majaliwa ya kocha Juma Mwambusi kujiunga nae kama kocha msaidizi yakiwa hayafahamiki.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.