Ligi Kuu

Kocha Simba: Kipindi cha pili wachezaji walipumzika.

Sambaza....

Licha ya Simba kupata ushindi mbele ya Kagera Sugar katika dakika za mapema lakini hawakumaliza vyema mchezo haswa katika kipindi cha pili.

Simba ilipata mabao mawili yote katika kipindi cha kwanza yakifungwa na Kibu Denis dakika ya 14 na John Bocco dakika 30 na kujihakikishia alama tatu mbele ya Kagera Sugar ambayo katika mchezo wa duru la kwanza walipoteza mchezo kwa bao moja bila.

Washambuliaji wa Simba Kibu Denis na John Bocco wakishangilia goli katika mchezo dhidi ya Kagera Sugar

Kocha Pablo alikiri timu yake ilicheza vyema kipindi kimoja tuu chakwanza na kushindwa kua na muendelezo mzuri katika kipindi cha pili na kupelekea Kagera Sugar kutawala mchezo.

“Ilikua ni ngumu ukizingatia kwamba hakukuwa na viungo wa asili kwenye eneo la ukabaji pamoja  na wale wa kutengeneza nafasi hivyo ilibidi nije kwa mtindo wa kipekee na tumeshinda mchezo wetu.” alisema Pablo

“Katika kipindi cha pili niliwaambia kwamba wanapaswa wapate muda wa kupumzika na kucheza kwa umakini,” Pablo Fanco kocha mkuu wa Simba

Baada ya ushindi huo Simba imefikisha alama 49, alama 8 nyuma ya vinara Yanga. Simba sasa wanajiandaa na mchezo wa Kombe la FA dhidi ya Pamba utakaopigwa katika uwanja wa Taifa.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.