Tetesi

Kocha Simba kutua Afrika Kusini.

Sambaza....

Aliekua kocha wa Simba Pablo Franco anahusishwa na kutimkia Afrika Kusini baada ya kutuma CV zake katika vilabu vikubwa nchini humo.

Kulingana na Kickoff magazine, Pablo Franco Martin ni miongoni mwa makocha wa kimataifa ambao wametuma CV zao kwa nafasi ya ukocha katika klabu ya SuperSport United ambayo iko wazi kufuatia kuondoka kwa Kaitano Tembo kabla ya mwisho wa msimu uliopita.

Pablo Franco Martin.

“Alikuwa kwenye orodha ya makocha pamoja na Marumo Gallants kule Orlando Pirates. Mambo hayakwenda sawa,” kilisema chanzo hicho.

“Anapatikana. Ana hamu ya kuja Afrika Kusini. Yuko wazi kwa fursa yoyote ya kuja kufanya kazi Afrika Kusini,” aliongeza. Shaun Bartlett

Pablo Franco.

Clinton Larsen na Fadlu Davids ni miongoni mwa makocha wazawa wanaowania nafasi ya ukocha katika SuperSport United pia pamoja na Franco Martin.

Sambaza....