Kocha wa klabu ya Simba Robertinho Oliveira
Mabingwa Afrika

Kocha Simba: Ni historia haikua rahisi.

Sambaza....

Simba imefanikiwa kuibuka na ushindi  mnono wa mabao saba katika mchezo wao wa Ligi ya Mabingwa Afrika na hivyo kufuzu kwenda robo fainali katika kundi C wakimaliza nafasi ya pili nyuma vinara Raja Casablanca.

Kocha mkuu wa klabu ya Simba Robert Oliveira amesema haikua jambo jepesi kupata ushindi mnono mbele ya Horoya katika mchezo ambao ulikua muhimu kwao kushinda na kwenda robo. 

 

Robert Oliveira “Kupata ushindi mnono wa mabao 7-0 katika Ligi ya Mabingwa sio jambo jepesi na wala haitokei mara kwa mara. Sisi tuliwasisitiza wachezaji wetu kuhakikisha tunacheza vizuri tukiwa hatuna mpira.

Nawapongeza wachezaji wangu kwa kuweza kufuata maelekezo tuliyowapa na kusababisha kupata ushindi huu.”

Robertinho Oliveira kocha wa klabu ya Simba

Mbrazil huyo aliwasifu wachezaji wake lakini pia amekiri kufurahi kwa kutimiza lengo la kufuzu kwenda robo fainali.

“Malengo yetu yalikuwa kuingia robo fainali na tunamshukuru Mungu tumefanikiwa hilo ndio jambo zuri la kujivunia,” alisema Robertinho Oliveira. 

Sambaza....