Nasradeen Nabi Kocha wa Yanga
Ligi Kuu

Kocha Yanga: Kesho tunacheza mechi mbili.

Sambaza....

Kuelekea mchezo wa Ligi Kuu ya NBC kati ya mwenyeji Dodoma Jiji na Yanga kocha wa Yanga ameonyesha kutilia mashaka ubora wa sehemu ya kuchezea ya uwanja wa Jamuhuri Dodoma.

Nasradeen Nabi kocha mkuu wa Yanga amesema kesho kutakua na michezo miwili mbele yake. Watakua wanacheza na Dodoma jiji pia watacheza na ubovu wa uwanja.

“Lakini kesho tunaweza kucheza mechi mbili tunacheza na  Dodoma Jiji lakini pia tunacheza dhidi ya uwanja tunajua kwamba viwanja haviwezi kufanana na Mkapa, Mbeya ama Morogoro lakini kuna changamoto za uwanja.” alisema Nabi.

Dodoma Jiji watakua wenyeji wa Yanga katika dimba la Jamuhuri Dodoma katika mchezo utakaopigwa majira ya saa kumi jioni.

Katika mchezo wa duru la kwanza Yanga waliibuka na ushindi wa mabao manne kwa bila dhidi ya Dodoma Jiji.

Yanga inashika nafasi ya kwanza ikiwa na alama 57 wakiwa hajapoteza mchezo wowote mpaka sasa na Dodoma jiji wapo nafasi ya nane wakiwa na alama 28.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.