Khalid Aucho wa Yanga akimdhibiti Pape Sakho
ASFC

Kombe la FA: Ni fainali ndani ya fainali.

Sambaza....

Kufuzu kwa Simba katika hatua ya nusu fainali ya Azam Sport Federation Cup maarufu kama ‘kombe la FA’ mara baada ya kuwabamiza timu kongwe ya Pamba mabao 4-0 kunaleta mtizamo wa kuona fainali mbili katika msimu huu.

Simba baada ya kufuzu wanakwenda kukutana na mahasimu wao Yanga ambaye alitangulia katika hatua hiyo baada ya kuwafunga Geita Gold kwa mikwaju ya penati.

Ukubwa na uzito wa mechi ya Simba na Yanga hakuna asiyoujua ni mechi itakayofunika thamani hali ya mchezo wa fainali kwa kuwa wakubwa hawa wanakutana katika hatua hiyo.

Naamini kama utawauliza mashabiki 10 wa mchezo wa mpira nchini Tanzania basi 9 kati ya hao angependa miamba hiyo ikutane katika fainali na si hatua hiyo.

Licha ya ukweli kwamba mkubwa yeyote atakayefuzu atakwenda kukutana na mshindi kati ya Azam au Coastal Union bado uzito wa fainali hiyo utapungua.

Kupungua huko kunatokana na mambo chungu mzima likiwemo tabaka la ubora kwa timu hizo mbili yaani Azam na Coastal Union dhidi ya wakubwa hawa Simba na Yanga.

Azam si yule unayeweza kumpa juu ya asilimia 50 za kushinda mchezo dhidi ya hawa kutokana na matokeo na mwenendo wa timu hii kwa sasa kifupi imekuwa ya kawaida sana

Nadharia hii inaweza kuthibitishwa na matokeo aliyonayo hasa kwenye maeneo mawili tu ya kuwiani wa michezo ya kushinda na kupoteza kwenye ligi kuu
ambapo amecheza michezo 23 na kupoteza 9 karibu na wastani wa michezo 2:1.

Djuma Shaban wa Yanga akimtoka kiungo wa Azam Fc Paul Katema.

Pamoja na ukweli michuano hii inatofautiana na FA ambayo inachezwa kwa mtoano lakini kuziaminisha akili za mashabiki kwamba ni mechi ngumu kwa yeyote atakaye ingia naye unaona haiwezekani

Coastal Union licha ya ukongwe wake na historia nzuri ya mafanikio siku za nyuma bado timu yao si bora kwenye maeneo mengi ndani ya uwanja na nje ya uwanja ili kuja kubattle na mkubwa yeyote ‘low professionalism’ na performance yao ikiwa inathibitishwa na matokeo yao katika michezo 23 wameshinda 7 wastani wa kupoteza 3:1.

Coastal Union.

Hivyo basi tutakubaliana mchezo wa nusu fainali kati ya Yanga na Simba ambao huwenda ukafanyika Arusha kutokana na maandalizi yanayoendelea katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid hii itakuwa na hadhi ya fainali kuliko fainali halisi.

Nusu fainali hii haijapangiwa tarehe na lakini endapo wanakutana sasa Simba wapo kwenye kiwango bora kuliko Yanga kutokana na matokeo wanayoyapata na uwezo wa kutikisa nyavu tofauti na wenzao waliopo kwenye mporomoko wa kimatokeo

Sambaza....