Michuano ya AFCON U17 itafanyika kwa mara ya kwanza Tanzania.
Mataifa Afrika U17

Kuelekea Afcon: tujikumbushe timu shiriki

Sambaza....

Kuelekea Afcon ya vijana chini ya umri wa miaka 17 itakayofanyika April 14 mpaka 28 jijini Dar es salaam tovuti yako ya kandanda.co.tz itakua inakuletea takwimu muhimu kuhusu michuano hiyo.

Michuano hii inafanyika kwa mara ya kwanza nchini Tanzania huku shukrani kubwa kwa raisi aliepita wa TFF Jamal Malinzi aliethubutu kuomba uenyeji na kufanikiwa kuupata.

Jumla ya timu nane zitatimua vumbi jijini Dar es salaam katika viwanja viwili. Viwanja vya Azam Complex-Chamanzi na uwanja wa Taifa- Kwa Mkapa ndivyo vitatumika katika fainali hizi.

Timu shiriki zitakua:

1. Tanzania

2. Uganda

3. Nigeria

4. Angola

5. Guinea

6. Cameroon

7. Morroco

8. Senegal

Makundi ya AFCON- U17 2019

Timu hizo zimegawanyika katika makundi mawili yaani kundi A na B. Ambapo washindi wawili (wa kwanza na wapili) kila kundi watapata nafasi ya kufuzu nusu fainali huku pia wakiwa wamekata tiketi ya kushiriki Kombe la Dunia la U-17 nchini Brazil.

#Kila Lakheri Serengeti Boys


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.