Masau Bwire msemaji wa Ruvu Shooting
Ligi Kuu

Kutufungia sisi ni sawa na kumpiga teke Chura- Masau Bwire.

Sambaza kwa marafiki....

Baada ya bodi ya ligi kuu kuvifungia viwanja vitatu kwa kutokidhi mahitaji ya club licencing, viwanja hivo ni Mwadui Complex unaotumiwa na Mwadui FC, Manungo unaotumiwa na Mtibwa Sugar, pamoja na uwanja wa Mabatini unaotumiwa na Ruvu Shooting.

Akizungumza na mtandao huu wa kandanda.co.tz, msemaji wa klabu hiyo ya Ruvu Shooting, Masau Bwire amedai kuwa wao kufungiwa ni sawa na kumpiga teke chura.

“Kutufungia sisi ni sawa na kumpiga teke chura, maana tulikuwa na mpango wa kujenga ukuta katika uwanja wetu wa mabatini”

“Kilichokuwa kinatukwamisha ni mkandarasi wetu ambaye yuko Marekani kwa sasa, tumekuwa tukimsubiri kwa muda mrefu sasa, lakini kwa sasa kuna vijana wetu wanahangaika kuzungusha ukuta na tunategemea mwezi wa tisa uwanja wetu utakuwa tayari na tutaanza kuutumia tena”- alisema Masau Bwire.

Wakati huo huo katibu mkuu wa Mwadui FC amedai kuwa walipewa taarifa hiyo muda mrefu na wamejipanga na watatumia uwanja wa Kambarage mkoani Shinyanga na wanaamini hapo wana mashabiki wengi.

“Tutatumia uwanja wa Kambarage mkoani Shinyanga, na hatuna shaka na hilo kwa sababu eneo hilo tuna mashabiki pia”.

Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.