Sambaza....

Mshambuliaji wa Liverpool Sadio Mane amewapa zawadi wakazi wa mji wa Bambali mjini Senegal (Mji aliokulia) wa fulana 300 kwa ajili ya kuzivaa wakati Liverpool itakapokuwa uwanjani kucheza na Real Madrid katika fainali ya Ligi ya Mabingwa wa Ulaya kesho.

Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 26 amegawa fulana hizo ikiwa ni kuongeza morali na mvuto wa mechi hiyo ya fainali ambapo Liverpool watakuwa wakichuana na mabingwa mara 12 wa taji hilo kubwa barani Ulaya kwa ngazi ya vilabu.

>>Ni Real Madrid tena? Au Liverpool?

“Wakazi wapo 2000 kijijini, lakini nimewanunulia Fulana 300 ili waweze kuzivaa wakati wakiangalia mechi ya fainali, Mama yangu na Mjomba wangu wote watakwenda kuungana na wakazi hao kuangali mechi, nimeambiwa hakuna mtu atakayefanya kazi siku hiyo, mimi nitaungana nao baada ya kombe la dunia, nina imani nitakuwa na medali ya ushindi na nitawaonesha,” Mane amesema.

Sadio Mane

Katika kijiji hicho ambacho familia yake inaishi ndipo ambapo Mane akiwa na umri wa miaka 13 alishuhudia Liverpool ikitwaa ubingwa mbele ya AC Milan mwaka 2005 katika fainali ya kukumbukwa sana na wapenda kandanda duniani kote.

Bofya picha kwenda kwenye utabiri
Bofya picha kwenda kwenye utabiri

“Nakumbuka AC Milan dhidi ya Liverpool, wakiwa nyuma kwa mabao matatu baade 3-3 na kuwapeleka kwenye penati na kuchukua taji, ilikuwa ni kumbukumbu kubwa kwangu,” Alisema Mane ambaye alikiri kuwa alikuwa ni shabiki wa Barcelona kipindi hicho.

“Kama kipindi hicho mtu angekuja na kuniambia kuna siku nitacheza fainali ya ligi, ningesema ni kitu cha ajabu katika maisha yangu, ninaimani tunaenda kushinda na kutwaa taji,” Mane alisema.

 

Sambaza....