Blog

Lipuli Wataambulia Mapato ya Mlangoni tu!

Sambaza....

Siioni Lipuli ikiambulia chochote licha ya kuwa na matokeo mazuri uwanja wa nyumbani, mbele ya Simba watapoteza alama zote tatu tena katika uwanja wao wa nyumbani bila shaka yoyote.

Simba ile iliyocheza na Mtibwa na makali yake yaliyowararua wakata miwa ndio pia itakayokwenda kuvunja Ngome ya “Wanapaluhengo” pale SamoraMeddie Kagere na John Bocco sioni nivipi watazuiliwa na safu chovu ya ulinzi inayoongozwa na Novat Lufunga chini ya mlinda mlango Deo Munishi

Kwenye kiungo kwa vyovyote vile naona uimara wa Jonas Mkude, Chama, Hassan Dilunga ukienda kuamrisha mchezo huku viungo wa Lipuli wakiendelea kukimbiza vivuli tuu.

 

Simba wakiwa katika mazoezi ya Mwisho kabla ya kukutana na Lipuli FC katika uwanja wa Samora

Tumaini pekee kwa Lipuli ni kwa Paul Nonga na Daruesh Saliboko ambao wanaweza kuitingisha na kupenya ngome chovu ya mabeki wa Simba chini Wawa, Shamte na Taroine Santos.

Hivyo basi kwa Lipuli kesho ni wazi wataambulia mapato ya getini tuu bila kupata alama yoyote kama hawakua makini kutumia udhaifu wa walinzi wa Simba.


Hizi ni mechi za leo na kesho za mzunguko wa pili. Kandanda tumekuwekea utabiri wetu wa kila mechi hapo chini. Unaweza kutupa na wewe pia

Utabiri Wetu


Wafungaji Bora

Na.MchezajiTimuNafasi
1Waziri JuniorMshambuliaji6
2Stephen Kwame5
3John R. BoccoMshambuliaji5
4Jordan JohnKiungo5

Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.