Tetesi

Lusajo aaga Namungo, kuibukia huku!

Sambaza....

Mshambuliaji kiongozi wa Namungo fc Reliant Lusajo ameandika ujumbe wa kuwaaga mashabiki na wachezaji wenzake wa Namungo fc katika ukurasa wake wa Instagram.

Lusajo baada ya kuzidengulia Azam, Simba na Yanga zilizokua zimeonyesha nia ya kuhitaji huduma yake sasa ni wazi njia nyeupe kuondoka Namungo fc.

Katika ukurasa wake wa Instagram ameandika hivi “Cha kwanza napenda kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kunipa uzima mpaka siku ya leo pili ningependa kutoa shukrani zangu za dhati kwa  uongozi pamoja na wachezaji wa Namungo kwa ujumla kwa muda wote tulioishi pamoja.

Ushirikiano mlionipa tangu kujiunga na timu Daraja la Kwanza mpaka hapa tulipofika, bila kusahau mashabiki wote wa Ruangwa waliokua wakitupa hamasa na support iliyotuwezesha kufikia malengo ya klabu. Nawatakia kila la kheri Mungu awabariki katika msimu ujao,”.

Kwa habari zilizo chini ya kapeti Reliant Lusajo huenda akaibukia moja kati ya timu zilizopanda daraja ambazo yupo katika mazungumzo nazo. Gwambina fc na Ihefu zinatajwa kutaka saini ya mshambuliaji huyo wa zamani wa Yanga.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.