Sambaza....

Baada ya klabu ya Simba kupoteza mchezo wake dhidi ya Mbao Fc kwa bao 1, kuna uwezekano klabu hiyo inaelekea kufanya maamuzi magumu lakini yenye maslahi si muda sasa.

Kwa mujibu wa ujumbe mfupi kutoka kwa Msemaji wa klabu hiyo, Hahi Manara, ameonyesha dhamira hiyo ikiwa pamoja na kuwaomba radhi kwa niaba ya uongozi wote  mashabiki wa wekundu hao wa msimbazi.


Bodi ya Wakurugenzi,Sekretarieti,Benchi la Ufundi na wachezaji wa klabu ya Simba,wanawaomba radhi Wanachama na Washabiki wetu kwa matokeo ya leo. Tumeumia sote na tunawaomba mjue hii ni mechi ya nne tu..tutafanya maamuzi sahihi bila pressure kwa maslahi MAKUBWA ya Timu na klabu..nawaomba mtulie ktk kipindi hiki.

-Haji Manara, Msemaji wa Klabu ya Simba.


Simba iliyochini ya Mbelgiji, Patrick Aussems, haina matokeo mazuri katika ligi kuu toka ianze kutoka nje ya Dar. Ilipata sare tasa dhidi ya Ndanda Fc kabla ya kutandikwa na Mbao Fc licha ya kumiliki mpira kwa asilimia nyingi.

Sambaza....