Ligi Kuu

Makata akisifu kikosi chake baada ya sare dhidi ya African Lyon.

Sambaza....

Kocha mkuu wa timu ya soka ya Alliance ya jijini Mwanza, Mbwana Makata amesema sare waliyoipata katika mchezo wa ligi dhidi ya African Lyon umetosha kabisa kuwaonesha wapi wapo na kitu gani wanatakiwa kukifanya ili kufanya vizuri katika ligi kuu msimu huu.

Amesema kikosi chake kimeweza kucheza vizuri katika mchezo huo tofauti na mchezo wa kwanza dhidi ya Mbao FC na kwamba wataendelea kufanya tathimini ili kujua namna wanavyoweza kuboresha zaidi kikosi chao.

“Cha msingi tumeshaiona ligi kwa mechi hizi mbili, tunaenda kufanya tathimini kujua ni jinsi gani ya kuweza kuperfome mechi zinazokuja, mimi bado nina imani na kikosi change ni kikosi kilichokuwa bora, nadhani kinapata uzoefu na kitakuja kutisha,” Makata amesema.

Akizungumzia kuhusu mchezo ujao ambapo itawalazimu kusafiri kwenda mkoani Mbeya kucheza na wajelajela Tanzania Prisons siku ya Septemba Mosi, Makata amesema anaamini wataenda kuibuka na ushindi katika mchezo huo.

“Plan yangu ni kwenda kushinda, sitaenda kupaki Bus, nitaattack muda wote na lolote linaweza kutokea ila itategemea na game siku hiyo itakuwa vipi na muonekano wake, na sisi tutabadilika kutokana na mchezo huo,” Makata amesema.

Baada ya michezo miwili Alliance FC ambayo imepanda ligi msimu huu, imekusanya alama moja baada ya kufungwa katika mchezo wa kwanza dhidi ya Mbao na kutoka sare dhidi ya African Lyon.

Katika mchezo dhidi ya African Lyon uliochezwa kwenye uwanja wa CCM Kirumba bao pekee la Alliance (The Rock Army) lilipatikana katika dakika ya 90 kupitia kwa Mnigeria Michael Chinedu baada ya kuonganisha mpira wa kona licha ya wachezaji wa African Lyon kulalamika kuwa kipa wao Tony Kavishe alisukumwa kabla ya kufungwa kwa bao hilo.

Sambaza....
Subscribe
Notify of

0 Maoni
Inline Feedbacks
Tazama Maoni Yote
0
Tungependa kupata maoni yako, tafadhali tuambiax
()
x