Mashindano

Mambo muhimu kuelekea siku ya Simba!

Sambaza....

Simba tayari wamezindua wiki yao ambayo itafika kilele siku ya August nane mwaka huu katika Dimba la Benjamin Mkapa ili kutizima utamaduni wao wa Simba Day.

Katika uzinduI huo ulihudhuriwa na wasanii, viongozi wa zamani na sasa wa Simba Sports Club. Baadhi ya mambo muhimu yalioyoongelewa siku hiyo Mbagala katika uzinduzi huo ni pamoja na haya.

“Kesho (leo) ndio mtajua kati ya msaada na udhamini, tutakua na tukio na mdhamini wetu mpya m-bet” Ahmed Ally msemaji wa klabu ya Simba

“Msimu huu tunarudi kwanguvu ili kutetea ubingwa wetu na tunakuja na “Hatushikiki, hatuzuiliki. Zoezi la usajili bado linaendelea idara yetu ya digitali itaanza kutangaza wachezaji kuanzia wiki ijao” Barbar Gonzales mtendaji mkuu wa klabu ya Simba

“Kuhusu jezi msimu huu tumeacha kwenda China, sasa jezi zetu zinatoka Ulaya hazitoki tena Asia na wiki hii tunazizindua,” Mwenyekiti wa Simba Murtaza Mangungu

“Nawapongeza wote mnaoendeleza hili jambo, hili jambo (Simba Day) nililianzisha mimi” Hassan Dalali Mwenyekiti wa zamani wa Simba
Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.