Blog

Manara aaga mapemaa..

Sambaza kwa marafiki....

Msemaji wa Mabingwa wa nchi (kama anavyojiita) Haji Manara amejikuta katika kigugumizi wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari uliofanyika leo katika hoteli ya Serena baada ya kuulizwa juu ya hatma ya nafasi yake ndani ya klabu ya Simba.

Manara ambaye amejizolea umaarufu  mkubwa kupitia kiti hicho, kutokana na staili yake kuwaunganisha wanasimba na klabu yao, amefunguka na kudai kuwa ni kweli nafasi hiyo ataicha kwani klabu imeshatangaza nafasi za kazi ikiwemo nafasi yake.

Manara amesema kuwa imekuwa ni tamaduni katika uongozi wowote wa taasisi au klabu kama Simba na zingine, wafanyakazi wake kufanya kazi kwa muda katika nafasi fulani na kisha kuwaachia wengine kushikilia nafasi hizo.

“ …Mimi nadhani kwa sasa ibaki kwamba msemaji wa Simba ni Haji Manara na kama itatokea vinginevyo ndio asili ya kazi hii.. na sina tatizo lolote na uongozi wa Simba…”

“.. Simba hii ni kubwa kuliko mtu yeyote yule… Simba ni kubwa kuliko haji..siku nitakayoondoka atakayekuwepo apewe ushirikiano na wanasimba wote kwa sababu Simba sio mali ya mtu mmoja…”

Klabu ya Simba katika kuboresha na kuleta weledi katika uendeshaji iliamua kutangaza nafasi za kazi ikiwemo nafasi ya Afisa Habari na mtendaji mkuu wa klabu, nafasi ambazo zinatarajiwa kupata warithi hivi karibuni.

Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.