EPL

Manchester United kumuongezea Mkataba Luke Shaw.

Sambaza....

Klabu ya soka ya Manchester United ya Uingereza imekubali kumuongeza mkataba beki wake wa kushoto Luke Shaw ambaye mkataba wake wa awali unakaribia kufikia kikomo mwezi Julai mwakani.

Taarifa zimesema Shaw mwenye umri wa miaka 23 anaweza kuongeza mkataba mrefu na mnono zaidi kuliko ule wa awali aliosaini mwaka 2014 akitokea Southampton kwa kitita cha Pound Milioni 27.

Mwanzoni kulikuwa na wasiwasi pengine mlinzi huyo ambaye amekuwa akikubwa na majeraha ya mara kwa mara angeondoka klabu hapo lakini kwa kiwango ambacho amekuwa akikionesha kwa siku za hivi karibuni zimeifanya bodi ya Manchester United kumfikira upya na kupanga kumuongezea mkataba.

Sambaza....
Subscribe
Notify of

0 Maoni
Inline Feedbacks
Tazama Maoni Yote
0
Tungependa kupata maoni yako, tafadhali tuambiax
()
x