Serie A

Mancini alaani vitendo vya kibaguzi kwenye soka.

Sambaza....

Kocha wa timu ya Taifa ya Italy Roberto Mancini amesema kitendo cha ubaguzi alichofanyiwa mshambuliaji kinda wa Juventus Moise Kean sio cha kuvumiliwa hata kidogo.

Mancini amesema adhabu kali na nzito inatakiwa kutolewa kwa mashabiki wa Cagliari ili kuzia tukio kama hilo ambalo limetokea kwa mara ya tatu ndani ya miaka mitatu mfululizo kwenye uwanja huo lisijirudie tena.

“Tabia hii haitakiwi kuendelea tena, inatakiwa hatua ichukuliwe na tena inatakiwa kuwa hatua kali, hata kule England ambao wapo mbali kwenye vita hii dhidi ya ubaguzi wa rangi matukio kama haya bado yanaendelea, lakini tunatakiwa kuunganisha nguvu na kuyaondoa kabisa michezoni,” Mancini amesema.

Mancini alimuita Kean kwa mara ya kwanza kwenye timu ya Taifa mwezi November mwaka jana na katika michezo ya kufuzu kwenye michuano ya Ulaya mwaka huu Kean mwenye umri wa miaka 19 alifunga mabao mawili katika michezo miwili waliyocheza.

Tukio la ubaguzi wa rangi kwa Kean lilitokea katikati ya juma hili ambapo Juventus walikuwa uwanjani wakipepetana na Cagliari na baada ya kufunga bao la pili kwenye dakika ya 85 Kean alikwenda kushangilia kwenye jukwaa la mashabiki wa Cagliari na ndipo walipoanza kuimba nyimbo za kibaguzi dhidi yake.

“Labda alitakiwa kufanya tofauti kidogo, Kean ni mchezaji wa kipekee, labda kwa wakati mwingine hatorudia kushangilia vile, nafikiri alikuwa amegadhabika,” Kocha huyo wa zamani wa Manchester City amesema.

Sambaza....
Subscribe
Notify of

0 Maoni
Inline Feedbacks
Tazama Maoni Yote
0
Tungependa kupata maoni yako, tafadhali tuambiax
()
x