Ligi Kuu

Mayele au Phiri, Top Scorer msimu huu.

Sambaza....

Kuna jamaa ananiambia mfungaji bora wa msimu NBC yupo miongoni mwa hawa jamaa wawili Mayele na Phiri.

Fiston Kalala Mayele

Mimi binafsi nambishia nikimwabia zamu ya Wazawa tena kama ilivyokuwa msimu uliopita nadhani wengi wanakumbuka.

Lakini pia moja ya Wachezaji wa kizawa hadi sasa ana ujumbe tofauti sana yaani Realint Lusajo mechi mechi 4 bao 5.

Nadhani vita ni vikubwa sana ila hapa kama watu wanachanganya madensa performance ya kwenye michuano ya kimataifa ( CAF) na huku kwenye NBC.

Lusajo

Licha ya miamba hii kuanza nao vyema ligi ya NBC kwa kupachika mabao kama upepo upo bora kwao kwenye Kimataifa zaidi mpaka sasa.

Tusubiri tuona huku tukipiga kura nani takuwa mfungaji bora miongoni mwa hawa na magoli unayotaraji kumaliza nayo.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.