Sambaza....

Timu ya soka ya Mbao ‘Wabishi’ kutoka jijini Mwanza wameendelea kufanya vyema katika msimu wa 2018/2019 wa ligi kuu soka Tanzania Bara baada ya jioni ya leo kuibuka na ushindi mwembamba wa bao 1-0 dhidi ya timu ya soka ya Tanzania Prisons.

Katika mchezo huo ambao ulikuwa wa kuvutia katika dakika zote 90, huku timu zikicheza zaidi mchezo wa nguvu na kiufundi, bao pekee la Mbao FC lilipatikana katika dakika ya 90 kupitia kwa mshambuliaji Mkongwe Ndaki Robert aliyeunganisha mpira wa faulo uliomshinda kipa Metacha Mnata na kujaa wavuni.

Kwa Mbao huu unakuwa mchezo wa pili mfululizo kushinda kwenye uwanja wao wa Nyumbani wa CCM Kirumba kwani ikumbukwe katikati ya Juma lililopita Mbao waliwafunga mabingwa watetezi Simba SC.

Matokeo hayo yanawafanya Mbao FC kukwea hadi kileleni mwa msimamo wa ligi wakiwa na alama 13, Alama moja mbele ya Mabingwa wa Kihistoria Yanga na alama tatu Mbele ya mnyama Simba SC ambaye ndiye bingwa mtetezi.

Matokeo katika Viwanja vingine.


Sambaza....