Mshambuliaji wa Yanga Fiston Mayele akizibitiwa na mlinzi wa Dodoma Jiji
Ligi Kuu

Mbinu mpya za Yanga zilizoacha lawama kwa kipa wa Dodoma Jiji

Sambaza....

Baada ya kutoka suluhu michezo mitatu na kumaliza dakika 270 bila bao lolote hatimae Yanga wanapata ushindi mbele ya Dodoma Jiji na kufuta jinamizi la sare na kurudi katika mbio sahihi za ubingwa.

Katika dimba la Jamuhuri Dodoma Yanga wanafanikiwa kuiadhibu Dodoma jiji na kuacha lawama kwa mlinda mlango Mohamed Yusuph aliesimama lango katika mchezo ule.

Zawadi Mauya na Fiston Mayele wakishangilia goli la pili dhidi ya Dodoma Jiji.


Baada ya kufeli kupata bao lolote katika michezo mitatu, kocha wa Yanga Nasredeen Nabi ilimlazimu kutoka katika mfumo wake wa siku zote wa kumtegemea Fiston Mayele na kubadili mbinu ili kupata ushindi.

Ni mbinu mpya ndio zilizofanya Jesus Moloko, Dickson Ambundo na Zawadi Mauya kuonekana na majukumu tofauti na muhimu kuliko kumzunguka Mayele.

Tazama hapa chini kuona jinsi Tigana Lukinja akiwachambua Yanga na goli la lawama alilofungwa kipa wa Dodoma Jiji.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.