Sambaza....

LIVERPOOL vs FULHAM, LIVERPOOL KUSHINDA

SABABU:

Mechi tano zilizopita, Liverpool ameshinda mechi 3 , akatoka sare mchezo mmoja na kupoteza mchezo mmoja. Wakati Fulham katika mechi tano zilizopita amefungwa mechi zote.

Mechi nne zilizopita kati ya Liverpool na Fulham , Liverpool wameshinda mechi zote. Na katika mechi nane dhidi ya timu zilizopanda ligi , Jurgen Klopp ameshinda mechi zote hizo.

Klopp (Kulia), meneja wa Liverpool akiwa na benchi la ufundi lake.

Mpaka sasa Liverpool haijafungwa katika mechi 29 zilizopita katika uwanja wake wa nyumbani. Rekondi ndefu kwao ya kwenda mechi nyingi bila kufungwa ni ya kwenda mechi 31 bila kufungwa nyumbani.


CHELSEA vs EVERTON, TIMU ZOTE KUFUNGANA.

SABABU

Timu zote ziko katika kiwango kizuri kwa sasa. Katika mechi tano zilizopita , Chelsea ameshinda mechi zote, wakati Everton kapoteza mechi moja tu na kushinda mechi nne.

Sarri, kocha wa Chelsea

Katika mechi tano hizo zilizopita , Everton imefanikiwa kufunga goli kwenye kila mechi. Ikiwa imefunga jumla ya magoli 12 na kufungwa magoli 6. Kwa hiyo hii inaonesha ina safu ya ushambuliaji ambayo inauwezo wa kufunga. Wakati Chelsea katika mechi tano zilizopita na yenyewe imefunga kwenye kila mechi, huku ikifunga jumla ya magoli 14 na kufungwa magoli 4. Kwa hiyo Timu zote zinasafu ya ushambuliaji zinazofunga na safu zao za ulinzi zinaruhusu magoli.


ARSENAL vs WOLVERHAMPTON WONDERERS, ARSENAL KUSHINDA

SABABU

Arsenal haijawahi kufungwa na Wolves katika mechi 16 zilizopita.Mara ya mwisho kwa Wolves kushinda dhidi ya Arsenal ilikuwa mwaka 1979.

Image result for arsenal fc

Arsenal imefanikiwa kuchukua alama 59 kati ya alama 63 dhidi ya Timu ambazo zimepanda daraja. Na Mpaka sasa Arsenal Haijafungwa katika mechi 9 zilizopita za ligi kuu.

Pia Arsenal wako nyumbani hii ni faida kubwa kwao. Msimu huu wamekuwa wakitumia vizuri sana uwanja wao wa nyumbani.


MANCHESTER CITY vs MANCHESTER UNITED, MANCHESTER CITY KUSHINDA

SABABU

Mechi tano zilizopita Manchester City ameshinda mechi zote, huku Manchester United akishinda mechi tatu na kufungwa mechi 1 huku akitoa sare mechi moja.

Na kwa msimu huu Manchester City imecheza dhidi ya top 6 mechi 3 , ambapo katika mechi hizo tatu ameshinda mbili na kutoka suluhu mechi moja. Mechi zote tatu dhidi ya wakubwa hajaruhusu hata goli moja.

Pep Guardiola

Wakati Manchester United msimu huu dhidi ya top 6 kacheza mechi mbili, ambapo amefungwa mechi moja dhidi ya Tottenham Hotspurs na kutoka sare dhidi ya Chelsea.

Kwa hiyo kwa msimu huu Manchester City dhidi ya mechi kubwa inaonekana ni nzuri kuzidi Manchester United na ikizingatia wapo katika uwanja wa nyumbani wa Manchester City (Etihad Stadium).

Sambaza....