Ligi Kuu

Mexime njiani kuelekea Yanga !

Sambaza....

Leo kulikuwa na mchezo wa ligi kuu kati ya Yanga na Kagera Sugar katika uwanja wa Uhuru , mechi ambayo imemalizika kwa Kagera Sugar kuifunga Yanga kwa magoli matatu kwa Bila.

Hiki ni kipigo cha kwanza cha kocha mpya Luc Eymael akiwa kama kocha mpya wa Yanga. Hii ilikuwa mechi ya kwanza katika Benchi la ufundi la Yanga.

Kabla ya mechi hii kulikuwa na taarifa kuwa Yanga walikuwa wanataka kuongeza kocha mwingine ambaye atasaidiana na Luc Eymael na kocha Charles Boniface Mkwasa.

Afisa Mhamasishaji wa klabu hiyo Antonio Nugaz alisema kuwa kwa sasa wanataka kuongeza kocha ambaye atasaidiana na benchi la ufundi lililopo kwa sasa la Yanga.

Kocha ambaye anasemekana kuja kuungana na benchi hili la ufundi la Yanga ni Mecky Mexime ambapo mpaka sasa hivi uongozi Wa Yanga uko katika mazungumzo naye ya kuja kwenye kikosi cha Yanga


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.