Blog

Mh. Magufuli abadili jina la uwanja wa Taifa!

Sambaza....

Mheshimiwa Rais Dr. John Pombe Joseph Magufuli leo katika shughuli za kumuaga aliekua rais wa awamu ya tatu marehemu Benjamin William Mkapa ameidhinisha Uwanja wa Taifa kubadilishwa jina na kuitwa uwanja wa Benjamin Mkapa.

Uwanja huo uliokua unajulikana kama Uwanja Mkuu wa Taifa uliopo pembezoni mwa uwanja mkongwe wa Uhuru una uwezo wa kuchukua jumla ya watazamaji 60,000 waliokaa kwenye viti.

Uwanja wa Benjamin William Mkapa!

Dr Magufuli “Nimetumiwa meseji nyingi na watu mbalimbali wakitaka uwanja uitwe kwa jina la Mkapa. Unajua Mzee Mkapa hakupenda vitu viitwe kwa jina lake, lakini leo hii amelala hapo hatoweza kunifanya chochote, basi kuanzia leo hii uwanja huo hapo mbele yenu utaitwa Uwanja wa Mkapa.”

Uwanja huo ulijengwa katika awamu ya pili ya uongozi  marehemu Benjamin Mkapa na kuanza kutumika mwaka 2007. Mpaka sasa uwanja huo unashika nafasi ya 11 kwa ukubwa barani Afrika.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.