Shirikisho Afrika

Micho awatamani wapinzani wa Simba!

Sambaza....

Kocha mkuu wa Uganda Milutin ‘Micho’ Sredojevic amejibu wito wa kurejea Orlando Pirates. Mashabiki wa Pirates hivi majuzi walijitokeza kwenye mitandao ya kijamii kumtaka mtaalamu huyo wa Serbia kurejea kwa wababe hao wa Soweto kwa mara yake ya tatu kuitumikia klabu hiyo.

Micho aliitumikia  “Buccaneers” mara mbili, lakini awamu yake ya mwisho ilizaa matunda zaidi alipoibadilisha Bucs kuwa washindani wa kudumu wa taji la PSL na kufika fainali ya Kombe la Telkom Knockout 2018.

Pirates  imekua katika kiwango cha kupanda na kushuka msimu huu chini ya makocha Mandla Ncikazi na Fadlu Davids jambo ambalo limesababisha baadhi ya mashabiki wa klabu hiyo kutaka watimuliwe.

Kocha wa Orlando Pirates Mandla Ncikazi

Alipowasiliana na Fast Post, Sredojevic alitoa ujumbe wa siri kwa kusema kwamba moyo wake, nafsi na akili yake viko kwa Pirates.

“Mwili wangu uko mbali na Orlando Pirates, lakini moyo wangu, roho na akili zipo. Ukishakua Pirates mara moja ni wakati wote unakua Pirates  hadi mifupa ioze.   

Mimi ndiye [kocha] pekee ambaye niliendelea kuwa shabiki.” Micho

Sredojevic Micho

Micho aliondoka Pirates mnamo Agosti 2019 baada ya kujiuzulu, akiwa amesimamia timu katika michezo 80 katika mashindano yote, akishinda 38, sare 26, huku akipoteza 16.

Lakiki muda mchache baadae alitangazwa kuwa kocha mpya wa Zamalek, lakini alifukuzwa chini ya miezi minne ya kazi yake mpya. Micho kisha alihamia Zambia ambako alihudumu kama mkufunzi wa Chipolopolo kwa miezi 16, kabla ya kuteuliwa tena kuwa kocha wa Uganda Julai 2021 kwa mkataba wa miaka mitatu. 

Cris Mugalu akimiliki mpira mbele ya wachezaji wa Orlando Pirates

Kikosi cha Pirates kimekua hakina kiwango kizuri msimu huu katika Ligi ya nyumbani lakini wakifanya vizuri katika Kombe la Shirikisho Afrika.

Pirates wana kibarua kigumu dhihi ya Simba katika mchezo wa marudiano baada ya kupoteza mchezo wa kwanza ugenini na huenda kutolewa na Simba katika michuano hiyo kukafanya kibarua cha Ncikazi kuota nyasi

Sambaza....