Zamani

Miroslov Klose alipoamua kuwa mkweli kwa goli la mkono

Sambaza....

Bila shaka dhambi inayoongoza ndani ya dimba la kandanda ni uongo. Ni kawaida mchezaji kuunawa mpira na akambishia refa kuwa hajashika. Kujiangusha kwenye box la 18 ili wapate penalty na danganya toto nyingine nyingi.Watu wa mpira wanalijua hili, haiitaji maelezo meengi!

Ni nadra sana kwa mchezaji wa mpira kukubali makosa, atabisha tu!

Ok! Turudi mwaka 2012 katika mechi ya ligi kuu ya Italia ya Serie A kati ya Napoli na Lazio. Miloslov Klose alifunga goli akiunganisha mpira wa kona.

Wakati wachezaji wenzake wa Lazio wakiendelea kushangilia, Klose alimfuata refa na kumwambia aliupiga mpira kwa mkono na kufunga.

Refa alibadili maamuzi ndipo wachezaji wa Napoli walimfuata Klose kumpongeza na kumshukuru kwa kuwa mkweli na muungwana.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.