Blog

Je kuna haja ya CCM kutafuta muwekezaji wa viwanja vyake?

Sambaza....

CCM yangu kwanini isitafute mwekezaji kwenye viwanja vya mpira ikiwa sehemu ya kuboresha mapato pia kuviweka viwanja vya mpira kwenye hali nzuri na kuvivutia vilabu vingine hasa vya DSM kuchagua viwanja vya mikoani.

Leo moja ya viwanja bora kabisa Tanzania wa ALI HASSAN MWINYI ulioko Tabora.
Ninapozungumzia ubora ni namna ya uwanja ulivyojengwa pia ukubwa na eneo la kuchezea “pitch”.
Ukiachana na uwanja wa ALI HASSAN MWINYI pia kuna uwanja wa NELSON MANDELA ulioko mjini Sumbawanga,Mkoani Rukwa.


Hiki nacho ni moja ya viwanja vizuri ambavyo vimesahaulika sana.

Vipo viwanja ambayo vinatumika sasa kwenye ligi za TPL,FDL na SDL ila navyo vina hali mbaya tu.
Matengenezo yake ni kama shinikizo la TFF/TPBL kuhakikisha uwanja unakuwa mzuri kwa matumizi ya ligi.

Leo hii kama tunaandaa AFCON U-17 ila michuano inafanyika ndani ya mji mmoja tu.
Wakati iliwezekana uwanja wa CCM Kirumba na hata Ali Hassan Mwinyi vingeweza kutumika kama tungekuwa na mazingira mazuri ya kuviendeleza hivi viwanja.

Harrison Mwakyembe waziri mwenye dhamana ya michezo

Natamani sana Waziri Mwakyembe aigeukie CCM kama Waziri mwenye dhamana ya michezo kuwaambia wa vikarabati hivi viwanja.
Akishindwa yeye basi Mwenyekiti CCM na Rais wa JMT Mheshimiwa Dkt Magufuli alisemee hili.

CCM ni rafiki wa vyama vya ukombozi n.k kwenye nchi mbalimbali ikiwepo China na kupitia ushirikiano huo kuna miradi mbalimbali inafanyika.
Sasa ni zamu ya viwanja hivi navyo kualika nchi rafiki watusaidie kuvikarabati.

Niwazavyo
Imeandaliwa na Jr Matukuta, UVCCM

Sambaza....
Subscribe
Notify of

0 Maoni
Inline Feedbacks
Tazama Maoni Yote
0
Tungependa kupata maoni yako, tafadhali tuambiax
()
x