Sambaza....

Klabu ya SimbaSc ya Dar es salaam imeendeleza wimbi la ushindi katika ligi kuu  (VPL) baada ya kuifunga Njombe Mji ya Njombe kwa mabao mawili kwa sifuri.

Mchezo huo uliokua mgumu kwa pande zote mbili, huku kila timu ikipambana kupata matokeo ili kujiweka nafasi nzuri katika ligi kuu Bara.

Simba vs Yanga Msimamo

PosTimuPWDLFAGDPts
12221554819439128311513
22151494422375126249491
32161225341328157171419
4214617776180211-31260
5216617481181231-50257

Alikua ni John Raphael Bocco “Mr Captain” alieamua mchezo huo baada ya kufunga mabao yote mawili na kuipa ushindi muhimu timu yake ya SimbaSc katika harakati za kuusaka Ubingwa wa Ligi Kuu Bara msimu huu.

Bocco alifunga goli la kwanza katika dakika ya 17 baada ya kupokea mpira mrefu uliopigwa na Yusuph Mlipili kabla ya kuutuliza na kupiga shuti kali nje ya 18. Mnamo katika dakika ya 68 Bocco tena alipokea pasi safi kutoka kwa Shomari Kapombe na kuukwamisha mpira wavuni.

Mpaka dakika 90 zinamalizika Njombe Mji 0 SimbaSc 2. Kwa matokeo hayo yanaifanya Simba kufikisha pointi 49 na kuwaacha Yanga wakiwa na point 46 akifwatiwa na Azam mwenye point 42.

Sambaza....