Sambaza....

Tajiri namba moja kijana Afrika na mfanyabiashara maarufu hapa nchini Mohammed Dewji amepatikana akiwa ameterekezwa katika viwanja vya Gymkhana Posta jijini la Dar-es-Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari kamanda wa kanda maamulumu wa Dar-es-Salaam, Lazaro Mambosasa amedhibitisha kuwa walipata taarifa kuwa Mohammed Dewji majira ya saa nane usiku katika viwanja vya Gymkhana.

Walipofika katika viwanja hivo vya Gymkhana walimkuta Mohammed Dewji akiwa ametelekeza pamoja na lile gari ambalo lilitajwa na IGP Simon Sirro likiwa limetelekezwa.

Kwa mujibu wa Mohammed Dewji “MO” ambaye ni shabiki wa Simba pamoja na mwenye hisa nyingi Simba amedhibitisha yuko salama, afya yake iko salama na watekaji mara nyingi walikuwa wanamsisitiza kuhusu suala la kula.

Muda wote aliokuwa ametekwa alikuwa amefungwa kitamba cheusi usoni ili kutojua sehemu alipo. Muda mwingi watekaji hao walikuwa wakisisitiza kupatiwa pesa na Mohammed Dewji. Lakini Mohammed Dewji alikuwa akiwasisitiza wampigie baba yake ili awapatie kwa sababu binafsi hakuwa nazo.

Jana IGP, Kamanda Simon Sirro alikuwa na mkutano na waandishi wa habari ambapo alitoa taarifa ya kulitambua gari ambalo lilikuwa limemteka mwanachama huyo wa klabu ya Simba, Mohammed Dewji.

Gari hilo ambalo lilitajwa na IGP, Simon Sirro ndilo gari ambalo lilikutwa likiwa limetelekezwa alfajiri hii katika viwanja vya Gymkhana, Posta Jijini Dar-es-Salaam pamoja na Mohammed Dewji, lakini gari hilo likiwa limebadilishwa “Plate Numbers” ambazo hazifanani na zile ambazo zilitajwa na Mohammed Dewji.

Tovuti ya Kandanda.Co.Tz. inayo furaha kubwa kwa upatikanaji wa Mohammed Dewji ambaye ni mdau mkubwa wa mpira hapa nchini. Hivo shukurani kubwa ziende kwa mwenyezi Mungu, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya Rais, John Pombe Magufuli, taasisi za dini zilikuwa zinamuombea pamoja na Watanzania wote. Pia tunatoa pole kwa familia ya Mohammed Dewji iliyopitia kipindi kigumu na Mungu azidi kuwatia nguvu kwenye kipindi hiki ambacho Mohammed Dewji kapatikana.

Sambaza....