Sambaza....

Mshambuliaji wa Liverpool  na timu ya taifa ya Misri jana alipata majeraha ya bega katika mchezo wa fainali jijini Kyiev dhidi ya Real Madrid.

Mchezo huo ulimalizika kwa Liverpool kupoteza kwa mabao matatu kwa moja mbele ya Real Madrid,  magoli ya Real Madrid yalifungwa na Karim Benzema na Gareth  Bale mawili.

Mo Salah aliumia katika kipindi cha Kwanza baada ya kuangushwa na beki wa Real Madrid  Sergio Ramos na kuangukia bega hivyo kumfanya ashindwe kuendelea na mchezo.

Salah akiwa chini baada ya kuangushwa na Sergio Ramos

“Ni majeraha ambayo yapo serious sana. Yupo hospitali anafanyiwa vipimo vya X-ray. Inawezekana ni mifupa ya begani. Hali yake sio nzuri kabisa” Kocha wa Liverpool Jurgen Klopp alisema baada ya mchezo kuisha.

Mpaka sasa ni vipimo vya matokeo ya X-ray ndio vinavyosubiriwa ili kuamua hatma ya Mo Salah kwenda kushiriki kombe la dunia nchini Russia. Mo Salah amekua mchezaji muhimu kwa timu yake ya taifa ya Misri hivyo kukosa fainali hizo itakua pigo kubwa kwao na kwa Africa kwa ujumla.

Sambaza....