EPL

Molde watoa msimamo mkali kwa Ole Gunnar.

Sambaza....

Klabu ya soka ya Molde ya nchini Norway imesema haina taarifa yoyote ya Manchester United kumuhitaji Kocha Ole Gunnar Solskjaer kwa kibarua rasmi, zaidi ya kuwa kocha wa muda.

Mkurugenzi wa Molde Oystein Neerland amesema wanatazamia Manchester United wataishi kwenye makubaliano ya awali na kwamba kocha Ole atarejea nchini Norway mwezi Mei kuendelea na kibarua katika klabu yake hiyo aliyoanzia maisha ya soka.

“Mwisho wa makubaliano ni May 12 mwaka huu, huo ndio mpango A na Mpango B sisi hatuna Mpango C kuhusu hilo, tumekubaliana na Manchester United kuhusu muda huu wa Januari hadi Mei, hakuna lingine zaidi ya hilo, na tutasimamia makubaliano ya awali,” Neerland amesema.

Ole Gunnar toka alipotua Manchester United baada ya kutimuliwa kazi kocha Jose Mourihno amekuwa na matokeo mazuri akishinda michezo yote mitano aliyoiongoza United, na jambo hilo limezidi kuwaumiza Molde kwani wamiliki wa United wanaweza kubadilisha mawazo na kumchukua mazima kocha huyo.

Mechi ijayo Manchester United watacheza na Tottenham ambayo inafundishwa na Mauricio Pochettino ambaye naye pia anawinda na Manchester United kwa ajili ya kibarua hicho, pengine matokeo ya mchezo huo yanaweza kubadilisha pia mtazamo wa United.

“Nafikiri Ole atarudi mwezi Mei, naamini” alimaliza Neerland ambapo wanatazamia kuanza michezo ya kabla ya Msimu siku ya Jumatatu bila ya kuwa na kocha wa mkuu.

Sambaza....
Subscribe
Notify of

0 Maoni
Inline Feedbacks
Tazama Maoni Yote
0
Tungependa kupata maoni yako, tafadhali tuambiax
()
x