David Molinga "Falcao"
Ligi Kuu

Molinga kuanza ligi rasmi Leo

Sambaza....

Kumekuwa na maneno mengi kuhusu David Molinga na uwezo wake. Wengi wamekuwa wakiamini David Molinga hastahili kucheza Yanga na wengine wanadai David Molinga anatakiwa kupewa nafasi zaidi.Kuelekea mchezo wa Leo wa ligi kuu kati ya Yanga na Polisi Tanzania utakaochezwa katika uwanja wa uhuru kumezungumzwa maneno mengi na Afisa Uhamasishaji wa klabu ya Yanga , Antonio Nugaz.

Antonio Nugaz amedai kuwa Leo hii David Molinga anaanza rasmi ligi kuu ya Tanzania Bara baada ya kapunguza uzito ambao ulikuwa unamsumbua.

“Tatizo lilikuwa uzito , na kwa sasa amepungua kwa asilimia kubwa kwa hiyo kuanzia kesho David Molinga ataanza rasmi ligi kuu Tanzania bara”-alidai Afisa huyo mhamasishaji wa Yanga.

David Molinga ni raia wa Congo. Mchezaji ambaye inasemekana alisajiliwa kwa mapendekezo ya mwalimu Mwinyi Zahera lakini mashabiki wengi hawajaridhika na kiwango chake.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.