Benard Morison "shibobo style"
Blog

Morrison awatosa Yanga , mbioni kwenda Simba

Sambaza....

Bernad Morrison ndilo jina ambalo kwa sasa ni chachu katika masikio ya mashabiki wa Simba , mashabiki ambao walifanywa watoke kichwa chini kwenye mechi iliyopita dhidi ya watani wao wa jadi Yanga.

Bernad Morrison ambaye amekuwa kipenzi kikubwa kwa mashabiki wa Yanga kwa sasa kutokana na kiwango chake kikubwa ambacho amekionesha tangu atue kwenye dirisha dogo la usajli msimu huu.

Leo hii mchezaji huyu amewaweka njia panda mashabiki wa Yanga na viongozi wa Yanga kwa ujumla baada ya kutopokea simu ya kocha mkuu wa Yanga , Luc Eymael.

Kocha huyo ambaye awali walikubaliana na Luc Eymael kuwa watasafiri kwa pamoja na Bernard Morrison kwenda Shinyanga kwenye mechi dhidi ya Mwadui FC .

Lakini kwa bahati mbaya Bernad Morrison hakupokea simu za viongozi wa Yanga pamoja na za kocha mkuu wa Yanga Luc Eymael. Hali ambayo imesababisha hali ya sintofahamu kwenye klabu ya Yanga.

Mtandao huu umepata tetesi kuwa Simba imekuwa ikimfukuzia kwa asilimia kubwa mchezaji huyo ili kumfanya acheze kwenye klabu hiyo ambayo kwa sasa ina ukwasi mkubwa kuzidi klabu nyingi hapa nchini.

Kutoka kwenye chanzo chetu cha ndani kimetupa tetesi hizo . “Nasikia Wakala wa Morrison yuko Dar na Yanga wameweka 70m jamaa aongeze mtataba na Bernad Morrison anataka 130 na 18m kwa mwezi”.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.