Benard Morison "shibobo style"
Ligi Kuu

Morrison kuufunika ufalme wa Deo Kanda?

Sambaza....

Kwasasa Yanga wana mtu wao wamemtoa Ghana ni mtaalamu kwelikweli wa kusakata Kandanda. Anafanya vitu vya msingi na visivyo msingi akiwa na mpira uwanjani, kwa maana anafanya vitu vya msingi vya kufuata maelekezo ya mwalimu na kuipa faidi timu na pia anafanya vitu visivyo vya msingi kwa kuwafurahisha mashabiki wa soka.

Benard Morrison winga mpya wa Yanga amekya gafla kipenzi cha mashabiki wa Yanga kwa michezo miwili tu aliyocheza mpaka sasa. Kwa kifupi ni mtaalamu wa mpira.

Mashabiki wa Yanga sasa wamekua wakitamba kuwa wamepata Deo Kanda wao, na hii ni baada ya mashabiki wenzao wa Simba waliokua wakitamba na uwezo wa winga wao Mcongo. Kabla ya ujio wa Morrison hakukua na shabiki wa Yanga aliekua akikiri hadharani uwezo mkubwa wa kiungo huyo wa pembeni wa Simba Deo Kanda.

Deo Kanda

Lakini baada ya ujio wa Morrison mashabiki wa Yanga wamekua wakisikika wakisema nawao wamepata Deo Kanda wao, kwa maana wamepata kiungo mahiri wa pembeni mwenye uwezo kama wake.

Mpaka sasa Deo Kanda ana mabao manne katika Ligi Kuu Bara, huku bao la mwisho akiwafunga Yanga katika sare ya mabao mawili kwa mawili katika dimba la Taifa.

Je Benard Morisson amekuja kuuzima ufalme wa Deo Kanda? Kwa lugha ya Malkia wanasema “Time will tell”, muda utaongea.

 


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.