Sambaza....

Mshambuliaji wa klabu ya Singida United, Eliuter Mpepo, ameongea na tovuti yetu kuelekea mchezo wao dhidi ya Ruvushooting na kusema wapo tayari kupambana na kutoka na alama tatu muhimu.

’Tutawapapasa wao leo, (huku akicheka), tumedhamilia kushinda ili tuwe katika nafasi nzuri katika msimamo” alisema Mpepo ambae mpaka sasa anagoli 2 Ligi Kuu.

Pia ametuahidi kufunga magoli zaidi na kurejea katika mbio za kuwania kiatu cha mfungaji bora kama ilivyokuwa msimu uliopita akiwa Tanzania Prison ambapo alimaliza na goli 7 na kutoa msaada magoli matano (5). Mpaka sasa Eliud Ambokile anaongoza kwa idadi ya Magoli kwa mwezi huu na Msimu huu.

Singida United mchezo wa mwisho imecheza jijini Mbeya, ambako ilitoka sare ya 0-0 dhidi ya Tanzania Prisons.

Sambaza....