Blog

Msimu huu Lipuli lazima tubebe kombe la FA

Sambaza....

Baada ya msimu jana kufanya vizuri kwenye michuano mbalimbali hapa Tanzania , timu ya Lipuli ya Iringa imesema lazima msimu huu imalize nafasi nne za juu na kuchukua kombe la chama cha soka Tanzania, Paul Nonga amedai kuwa wamejiandaa vizuri msimu huu kuzidi msimu jana.

“Wanasema ukishindwa kujipanga basi umejipanga kushindwa, sisi tumejipanga kushinda kabisa msimu huu. Msimu huu tumepanga tumalize katika nafasi nne za juu na kuhakikisha tumebeba kombe la FA ambalo msimu jana tulifika fainali.

Alipoulizwa na mtandao huu kuhusu mafanikio ya msimu jana yalivyo na nafasi ya kufanya vyema msimu huu , Paul Nonga amedai mafanikio ya msimu jana yametupa moyo sana.

” Msimu jana tumefanya vizuri sana. Kwa hiyo huu umekuwa kama mtihani kwetu kwa sababu kila mtu anataka kutuangalia namna ambavyo tutakavyofanikiwa zaidi ili watu wajue kabisa hatukubahatisha kwa mafanikio ya msimu Jana. Na tumejiandaa vizuri zaidi kuzidi tulivyojiandaa msimu Jana”- alisema Paul Nonga.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.