Bakari Nondo Mwamunyeto
Tetesi

Mwamunyeto kumbe kashamwaga wino tayari!

Sambaza....

Mlinzi wa Coastal Union na Taifa Stars Bakari Nondo Mwamunyeto ambae amegeuka lulu kwa Simba na Yanga katika usajili ujao kumbe tayari ameshaamua ni wapi atatumikia msimu ujao wa 2020/2021.

Mwamunyeto ambae amebakisha mkataba wa mwaka mmoja na Coastal Union kati ya minne aliyosaini tayari wameshakubaliana kila kitu na Wanajangwani chini ya tajiri wao GSM. Kinachosubiriwa ni Ligi tuu kumalizika na usajili kufunguliwa rasmi.

Raphael Obafemi wa Mwadui fc akipambana na Bakari Mwamunyeto wa Coastal Union.

Mtoa taarifa ambae hakupenda jina lake litajwe amesema Bakari amesaini Yanga tayari kutokana na makubaliano mazuri yaliyofikiwa kati ya Coastal Union, Mwamunyeto na GSM ambao ndio waloofanikisha dili kwa niaba ya Yanga.

Msimu ujao Coatal watavaa jezi zenye udhamini wa GSM ikiwa ni sehemu ya makubaliano ya kuvunja mkataba wa mwaka mmoja uliobaki wa Mwaminyeto huku kiasi cha fedha atakachopokea Mwamunyeto mwenyewe kikibaki kua ni siri.

Sambaza....