Ligi Kuu

Ni mapema mno kumfukuza kocha wa Simba

Sambaza kwa marafiki....

Moja ya kelele ambazo kwa sasa zinapigwa na mashabiki wa Simba ni wao kutomtaka kocha wao mkuu wa sasa.

Wanaamini timu yao inacheza soka ambalo siyo la kuvutia na soka ambalo linawafanya wao kuhangaika kupata ushindi kwenye mechi zao.

Kabla ya kufungwa mechi ya jana , Simba walienda mechi nne mfululizo wakitanguliwa na timu pinzani kabla ya kusawazisha na kushinda.

Lakini pamoja na kwamba Kocha mkuu wa Simba analalamikiwa Sana , Lakini takwimu zinambeba na kuonesha kuwa yuko kwenye mstari ambao ni sahihi.

Katika mechi 10 ameshinda mechi 8, sare 1 kipigo kimoja, magoli 23,  takwimu ambazo zinambeba sana na kumfukuza ni sawa na kumuonea kwa sababu ya takwimu zinavyombeba.

Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.