Ligi

Nimeshakomaa, lazima niwafunge Simba-NCHIMBI

Sambaza....

 

Baada ya tetesi zilizokuwa zimeeenea kuhusu uhamisho wa Ditram Nchimbi kutoka Azam FC kwenda Yanga kwa uhamisho wa milioni 20 , Leo hii tetesi zimekamilika na kuwa kitu halisi , Ditram Nchimbi ni mchezaji halali wa Yanga.

Safari ilianzia nchini Uganda , mmoja wa wadhamini wa Yanga , GSM amesafiri mpaka Uganda kwa ajili ya kukamilisha uhamisho huo. Akizungumza Baada ya usajili huo , mdhamini huyo amedai kuwa wanachokifanya ni kinyume na mkataba wao.

“Usajili ni kinyume na mkataba wetu , mkataba wetu haututaki kufanya usajili lakini tunafanya hivi kwa sababu ya mapenzi tuliyonayo kwa Yanga. ” Jana Ditram Nchimbi , Azam, Police na Yanga wamemaliza tofauti ambayo ilikuwa inamzuia Nchimbi kuwa mchezaji halali wa Yanga

Naye Ditram Nchimbi amedai kuwa amefurahia kusajiliwa Yanga kwa sababu wachezaji wengi hutamani kusajiliwa Yanga. “Nimefurahia kusajiliwa Yanga , wachezaji wengi hutamani kusajiliwa na Yanga”.

Kuhusu mechi ya tarehe 04/01 mwaka huu dhidi ya watani wa jadi, Ditram Nchimbi amedai ataonesha ukomavu wake. “Watu wengi wanasema sijakomaa, kwenye mechi hii nitawaonesha watu ukomavu wangu kwa kuifunga Simba” amedai mchezaji huyo mpya wa Yanga.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.