Tetesi

Nyota 13 watakaoachwa Yanga kujulikana!

Sambaza kwa marafiki....

Klabu ya soka ya Yanga baada ya kuanza usajili kwa kasi baada ya dirisha la usajili kufunguliwa August 01 kwa msimu ujao pia inatarajia kutangaza wachezaji watakaochwa kuelekea msimu ujao.

Za chini ya kapeti inasemekana kesho Klabu ya Yanga itatangaza nyota 13 ambao itaachana nao kabla ya kuanza kwa msimu ujao. Huku pia sababu mbalimbali za kuwaacha nyota hao zikiwekwa wazi.

Miongoni mwa sababu hizo ni pamoja na utovu wa nidhamu kwa wachezaji, viwango vibovu vya wachezaji pamoja na wale wanaoonekana waanzilishi wa migomo.

Baadhi ya nyota wataoachwa ni pamoja na Yikpe, Molinga, Raphael Daud, Andrew Vicent, Ally Ally,Adeyum Saleh, Paul Godfrey, Ally Sonso.

Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.