Blog

Parimatch waingia mkataba na Mbeya City.

Sambaza....

Kampuni ya michezo ya kubashiri ya Parimatch imeingia mkataba wa mwaka mmoja wa kuidhamini na klabu ya Mbeya City ambao utaanza katika msimu huu wa 2022/2023.

Wakizingumza mbele ya Waandishi wa Habari wawakilishi wa kampuni ya Parimatch na viongozi wa Mbeya City wamekiri kuwa na furaha kwa pande zote mbili kuingia katika ushrikiano huo ambao ni wa mwaka mmoja huku pia kukiwa na nafasi ya kuongeza mwingine.

“Kampuni yetu ina miaka mitano hapa nchini Tanzania lakini tunafanya kazi katika nchi kumi na tano duniani. Tunafanya kazi na vilabu vikubwa duniani ikiwemo Leicester City na Chelsea  za England.” Ismail Mohamed afisa habari wa Parimatch.

“Tunapenda kuutaarifu umma kua leo Jumanne August tarehe 9 mwaka 2022 tumeingia mkataba na klabu ya Jiji la Mbeya Mbeya City ambayo inashiriki michuano ya Ligi Kuu Bara kwa msimu huu wa 2022/2023.  Mkataba huu ni wenye faida kwa pande zote mbili,” aliongeza Ismail

Nae Katibu Mkuu wa Mbeya City amewahakikishia wadhamini wao wapya kampuni ya kubashiri Parimatch wapo sehemu sahihi na kuahidi kuwa na mchezo mzuri wakitumia mtaji mkubwa wa mashabiki walionao.

” Tunashukuru uongozi wa Parimatch kwa udhamini huu na tunawakaribisha sana Mbeya. Tuna mashabiki wengi zaidi nchini ukiondoa timu hizi mbili kubwa.” Kimbe

” Msimu uliopita tulicheza bila mdhamini lakini tunashukuru wamerudi, tutawapa kila wanalostahili katika kutimizia masharti ya mkataba. Lakini pia tunawaahidi msimu huu tutafanya vizuri katika Ligi na tutamaliza katika nafasi nne za juu,” Emmanuel Kimbe

Mkataba huo ni wa mwaka mmoja wenye kipengele cha kuongeza mwaka mwingine pia. Pamoja na pesa taslim (itabaki kuwa bayana baina ya pande husika) Parimatch itatoa vifaa kwa klabu pamoja na ukarabati mdogo wa uwanja wa Sokoine.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.