Kevin Kongwe Sabato "Kevi Kiduku".
Ligi Kuu

Pesa za Kagera nisingeweza kuziacha- Kevi Sabato

Sambaza....

Galacha wa mabao wa mwezi February Kevin Kongwe Sabato “Kevi Kiduku” wa Kagera Sugar ametoa ya moyoni kuhusiana na uhamisho wake wa kutoka Gwambina fc na kutimkia kwa Wanakurukumbi Kagera Sugar.

Kevi Kiduku mwenye mabao saba mpaka sasa ambae alijiunga na Kagera katika usajili wa dirisha dogo akitokea Gwambina ya daraja la kwanza.

Baada ya kuachana na matajiri wa Gwambina na kujiunga na Kagera Sugar tovuti yako pendwa ya Kandanda ilitamani kujua ni kwanini aliamua kuhamia timu hiyo ya VPL.

Zawadi ya mvinyo na kiatu alichokabidhiwa Kevin Kongwe Sabato kwa kuibuka Galacha wa mabao kwa mwezi February!

Kevin Sabato “Ni mzigo tuu hakuna kingine, Kagera Sugar walifika dau na ndio maana ikawa rahisi mimi kujiunga nao. Kagera Sugar ni timu nzuri na zoefu Ligi Kuu Bara lakini pia ina mwalimu mzuri katika Ligi yetu hivyo pia haikua ngumu kwangu kuja hapa.”

Mshambuliaji huyo wa zamani wa Abajalo fc, Mwadui fc na Mtibwa Sugar pia ametaja goli ambalo mpaka sasa analikumbuka na huwa analikumbuka sana katika maisha yake

Kevin Sabato akiwa na zawadi zake baada ya kuibuka Galacha wa mabao kwa mwezi Februari

Sabato “Goli nililowafunga Mbeya City wakati naitumikia Majimaji fc ya Songea lilikua bora na muhimu sana katika mchezo ule  hakika nalikumbuka sana. Katika dimba la Majimaji Songea game ilikua sare ya bao moja kwa moja na ilikua lazima tushinde mchezo ule.

Nilipokea mpira kwa kifua nikiwa katikati ya mabeki wawili wa Mbeya City, Tumba Swedi alitegeana na mwenzake wakajua nitautuliza tena lakini nilipiga shuti vilevile na mpira ukaingia wavuni. ”

 

 


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.