EPL

Pogba: Naenjoy soka United!

Sambaza....

Kiungo wa Manchester United amesema anafurahia kwa jinsi wanavyocheza mpira akiwa na United, huku pia akiwamwagia sifa wachezaji wenzake anaocheza nao haswa eneo la kiungo na ushambuliaji.

Pogba ambae amekua akiingia katika mikwaruzano ya mara kwa mara na benchi la ufundi la United huku pia wakala wake akiweka wazi Mfaransa huyo anataka kuondoka United, klabu za Juventus na Real Madrid zimekua zikitajwa kutaka huduma yake.

Paul Pogba na Bruno Fernandes!

“Unaweza kusema kwamba timu imebadilika sana. Tunacheza kama timu kuliko vile tulivyofanya hapo awali, tunafurahia zaidi, tunakaba kwa pamoja, tunashambulia pamoja, na timu ina nguvu pia.

“Kutoka eneo la ulinzi ninafurahia sana. Ninaenjoy kumtazama Bruno, [Marcus] Rashford, [Anthony] Martial na Mason [Greenwood], ambao wote walicheza mchezo wa mwisho, na kuwaona wakifunga mabao. Unaendelea kupata shangwe, ni nzuri. Inanifanya nifurahie mpira kila wakati.” Paul Pogba aliiambia United Review.

Sambaza....