Wachezaji wa Yanga wakiwa kwenye gari maalum wakipita mitaani Jijini Dar es salaam
Ligi Kuu

Rais FIFA aguswa na ubingwa wa Yanga!

Sambaza....

Rais wa Shirikisho la Soka Ulimwenguni FIFA Gianni Infantino ameonekana kuguswa na kutoa pongezi kwa kabu ya Yanga baada yakutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya NBC katika msimu wa 2021/2022.

Infantino amesema ubingwa huo umekuja kutokana na juhudi za kila mmoja katika klabu ya Yanga na wote wanapaswa kujivunia kutokana na ushindi huo. Infantino ameyasema hayo kupitia barua aliyotumia nchini kupitia Shrikisho la Soka TFF.

Aidha rais Infantino pia ameonyesha kuheshimu na kumshukuru Rais wa TFF Wallace Karia kwa juhudi zake kubwa katika kukuza mchezo wa soka katika Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati [CECAFA].

Klabu ya Yanga imefanikiwa kutwaa ubingwa wake wa 28 wa Ligi Kuu Bara msimu huu baada ya kukaa bila ubingwa kwa misimu minne mfululizo.

Sambaza....