Blog

Sadio Kanoute na kisasi cha Ronaldinho

Sambaza....

Unamkumbuka Ronaldinho Gaucho akiwa kwenye kiwango bora kabisa pale Milan, Barcelona na Brazil? Alikuwa ni miongoni mwa wachezaji waliochezewa madhambi mengi kwenye kila mechi.

Ronaldinho hakujali aliinuka na kutabasamu kisha kuendelea kuwatesa viungo na mabeki wa timu pinzani huku akitabasamu tu. Yaani anakuua huku anacheka.

Ronaldinho Gaucho.

Sahau kuhusu Ronaldinho, rudi Dar es Salaam Tanzania ndani ya kikosi cha Simba kuna kiungo Mmali anaitwa Sadio Kanoute, wenyewe wanamuita ‘Putin’.

Huyu ni kiungo haswa lakini ukimuona kimoyo moyo utasema “Jamaa mbona kama analipa kisasi kwa Ronaldinho.!🤔”

Wakati Ronaldinho muda mwingi akionekana kutabasamu, Kanoute yeye muda mwingi amenuna, hatabasamu wala kucheka kizembe. “Mkimuona njoo mnipige nimekaa pale kiduka cha mangi😎”.

Sadio Kanoute “Putin”

Kwa wanaoishi na Kanoute wanamuelezea kama mcheza soka mwenye nidhamu, upendo na roho safi licha ya muda wote kuonekana kununa.

Muonekano wake huo umewafanya wachezaji wenzake kumpa jina la ‘Putin’ wakimfananisha na Rais wa Urusi mwamba Vladmir Putin. (Hawana mzaha).

Kanoute ni kiungo wa mifumo. Namba zake eneo la kiungo ni kubwa sana pale Simba lakini wanazijua sana wajuzi wa soka, makocha na wachezaji wenzake kuliko mashabiki oya oya.

Sadio Kanoute akichukua mpira mbele ya wachezaji wa Asec Mimosa.

Huenda muonekano wake wa ‘kununa’ ukawa tofauti na uhalisia wa nafsi yake. Nafsi inacheka tu bila wasi wasi.

Kanoute anavunja kuni, anakaba, anapiga pasi pia anafunga. Simba inaenjoy kuwa naye katika kikosi chake lakini ukiachana na yote hayo, KUNUNA ni utambulisho mwingine wa Kanoute kwenye dunia ya Soka.

NB: Kanoute ni nani? Yule mchezaji wa Simba asiyecheka kizembe.

Sambaza....