Sambaza....

Daktari wa klabu ya soka ya Liverpool Ruben Pons amethibitisha kuwa mshambuliaji Mohamed Salah hatofunga Ramadan leo wala kesho katika kuelekea mchezo wao wa fainali ya ligi ya Mabingwa barani Ulaya dhidi ya Real Madrid.

Salah ambaye ni Muislam alikuwa katika mfungo toka Mei 16 lakini sasa imebainika kuwa hatofunga ambapo kwa mujibu wa sheria za dini inaruhisiwa kufanya hivyo lakini kama kutakuwa na sababu muhimu kwa muumini.

Kutokana na wengi kuwa na wasiwasi kuwa kama angefunga ingeleta shida kwake katika mchezo wa kesho utakaofanyika Mjini Kiev nchini Ukraine, basi hofu hiyo imeondolewa rasmi kwani Salah atakuwa fit zaidi

Dokta Pons ameiambia Radio ya Uhispania Cadena SER, kwamba Salah atakula kama kawaida leo pamoja na kesho ukiwa ni mpango mkakati kumuwezesha kuwa kamili kabla la kucheza na Real Madrid.

“Ijumaa na siku ya mchezo hatofunga, kwa hiyo haitamuathiri chochote,” alisema Dokta huyo huku pia akithibitisha kuwa wachezaji Sadio Mane pamoja na Emre Can ambao pia ni Waislam wataendelea na mfungo kama kawaida.

Sambaza....