Mchezo wa mwisho wa Simba Kimataifa
Stori

Saudi Arabia Kumwaga Mamilioni kwa Simba Sc.

Sambaza....

SAUDI ARABIA iko kwenye mazungumzo na Shirikisho la Soka barani Afrika (CAF) juu ya mpango wa dola milioni 200 (zaidi ya bilioni 400) ili kudhamini Ligi mpya ya Afrika, katika makubaliano ambayo yanaweza kusaidia kupata uungwaji mkono wa bara hilo kwa ombi lolote la Kombe la Dunia. 

CAF ilipaswa kuzindua michuano hiyo ya timu 24 ambayo imeungwa mkono kwa kiasi kikubwa na rais wa FIFA, Gianni Infantino, mwezi Agosti, kama sehemu ya mipango ya kuinua hadhi ya kimataifa ya vilabu vya Afrika na kuongeza mapato. Super League, iliyopendekezwa kwa mara ya kwanza na Infantino mwaka 2018 na kutangazwa na rais wa CAF Patrice Motsepe mwezi Oktoba.

Michuano hiyo imepangwa kuwa na fedha ya zawadi ya dola za Marekani milioni 100 ambazo ni pamoja na dola za Marekani milioni 11.6 (zaidi ya bilioni 23 za Kitanzani)  kwa mshindi ambazo ni zaidi ya  karibu dola za Marekani milioni 8 (zaidi ya bilioni 16 za Kitanzania) zaidi ya anachopata mshindi wa Ligi ya Mabingwa Afrika. 

Patrice Motsepe, Rais wa CAF.

Mazungumzo na Saudi Arabia yanaaminika yamekuwa yakiendelea kwa muda na wiki mbili zilizopita, CAF ilitangaza kuwa wametia saini mkataba wa miaka mitano wa ushirikiano na maendeleo na Shirikisho la Soka la Saudi Arabia.

“CAF inafuraha kufanya kazi pamoja na kushirikiana na Shirikisho la Soka la Saudi Arabia kuendeleza na kukuza soka katika bara letu na kimataifa,” alisema Motsepe katika taarifa yake. “Pia kuna maeneo mahususi ya ushirikiano wenye manufaa kwa pande zote mbili ambayo tunajadili na taarifa itatolewa kwa wakati ufaao.”

Saudi Arabia imekuwa katika harakati zakutaka kuandaa michuano ya Kombe la Dunia 2030 licha ya sheria za FIFA kuzuia mataifa ya Shirikisho la Soka la Asia kuandaa Kombe la Dunia la Wanaume hadi 2034, baada ya kuchaguliwa kwa Qatar kwa mashindano ya 2022.

Kikosi cha Simba Sc.

Nchi hiyo ya Kiarabu inatazama bara la Afrika kama sehemu ambayo wanaweza kupata uungwaji mkubwa mkono katika harakati zao hizo na ndio maana wanaendelea kuweka mahusiano na shirikisho la soka Afrika CAF. 

Endapo mpango huo utatimia ni wazi klabu ya Simba itafaidika na mamilioni hayo kwani mpaka sasa ndio timu pekee kutoka Tanzania ndio itakayoshiriki michuano hiyo mipya kabisa Afrika kwa ngazi za vilabu.

Sambaza....