Sambaza....

Timu ya Taifa ya vijana yenye umri chini ya miaka 17 “Serengeti boys” imepata mualiko barani Ulaya katika nchi ya Uturuki mapema mwakani.

Mabingwa hao wa kombe la COSAFA, Serengeti boys wamepata mualiko katika michuano maalum iliyoandaliwa na shirikisho la mpira barani Ulaya na la Africa pia (UEFA&CAF)  yanayotarajiwa kufanyika nchini Uturuki mapema February mwaka 2019.

Mashindano hayo yatakua maalum kwaajili ya Serengeti boys kujiandaa na Afcon ya vijana wenye umri chini ya miaka 17 ambapo Tanzania itakua mwenyeji wa mashindano hayo kwa mara ya kwanza.

Michuano hiyo inatarajiwa kuanza mapema February 22 mpaka March 2 na kuzishirikisha timu 12 kutoka mataifa mbalimbali kutoka barani Ulaya na Africa. 

Sambaza....