Ligi Kuu

Simba hii haitanii, yaitwanga Mtibwa kwake.

Sambaza....

Kikosi cha Simba kimeonyesha hakitanii na wanataka ubingwa kweli wa Tanzania Bara baada ya kupata ushindi dhidi ya timu ngumu ya Mtibwa Sugar katika uwanja wa Jamuhuri Morogoro.

Simba wamefanikiwa kuibuka na ushindi wa bao moja na kupata point tatu muhimu kuelekea kutwaa ubingwa wa VPL. Goli lá Simba lililofungwa na Emmanuel Okwi katika dakika ya 24 baada ya kazi nzuri ya Shiza Kichuya na John Bocco.

Mtibwa Sugar waliokua nyumbani walijitahidi kwa kiasi kikubwa kusawazisha goli bila mafanikio huku kikwazo kikubwa wakiwa walinzi wa Simba wakiongozwa na Aishi Manula akisaidiwa kwa kiasi kikubwa na Yusuph Mlipili na Paul Bukaba aliecheza mechi yake ya tatu ya Ligi.

Kwa ushindi wa leo unaifanya Simba kuendelea kuongoza ligi wakifikisha point 52 na kuwaacha Yanga kwa alama 6 ambao wana mchezo dhidi ya Singida utd Katika uwanja wa Taifa Dar es salaam.

Kikosi Cha Mtibwa kilikua: Tinoco, mganga, kibwana, Isihaka, Daud, Nditi, Kihimbwa, Shindika, Mbonde/Javu، Dilunga/Chanongo, Mhesa/ Semtawa.

Kikosi cha Simba kilikua: Manula, Gyan/Niyonzima, Kwasi, Bukaba, Mlipili, Mkude, Kapombe, Mdhamiru/Mbonde, Bocco, Okwi, Kichuya.

Sambaza....
Subscribe
Notify of

0 Maoni
Inline Feedbacks
Tazama Maoni Yote
0
Tungependa kupata maoni yako, tafadhali tuambiax
()
x