Shirikisho Afrika

Simba hii ni tofauti itafuzu nusu fainali!

Sambaza....

Simba wamewasili salama nchini Africa kusini kwenye mchezo wao wa marudiano dhidi ya wenyeji wao Orlando Pirates ambapo kwenye mchezo wa awali Lunyasi walitakata kwa ushindi bao 1-0.

Binafsi nina mtazamo tofauti na walio wengi kwamba Simba wanaenda kutolewa lakini kwangu naamini Lunyasi wanaenda kufuzu nusu fainali ya kombe la shirikisho.

Kwanini naamini hivyo basi? Najua hakuna tendo gumu kwenye mchezo wa soka kama kudumbukiza mpira wavuni, Simba kashafanikiwa mchezo wa kwanza kufanya hivyo.

Shomary Kapombe akifunga penati iliyoipa ushindi Simba mbele ya Orlando Pirates.

Orlando analazimika kupata goli, hili ni jukumu lake la lazima kama atataka kufuzu hana jinsi ‘atake asitake itakuwa hivyo’ kitu ambacho ni tofauti na wapinzani wao Simba Sports.
Simba ametoka kwenye jukumu la kuhitajika goli ama kutikisa nyavu kutokana na mtaji aliona kibindoni.

Suluhu yeyote itamfanya afuzu hana deni na goli hadi tu atakaporuhusu goli yeye naamini Simba wanaweza kutengeneza muunganiko mzuri utakaofanya nyavu zao zisitikiswe kwa dakika 90 na hili linawezekana.

Kwa kile nilichokiona kwenye game ya kwanza pale Estadio De Mkapa yote yanawezekana Orlando hawakuonesha utundu maarifa zaidi nje ya “team combination” kwa maana timu zinazocheza hivi ni rahisi kuzithibiti.

Kibu Denis akipiga shuti mbele ya walinzi wa Orlando Pirates.

Simba anatakiwa akaugawe muda vizuri ndani ya dakika 90 asiruhusu goli la mapema wafanye juhudi nyingi na kukaba kwa principle zote 3 Man to man, zone marking na compact marking.  Kifupi wafanye kazi mithili ya “siafu” wanaomjengea malkia nyumba yake.

Kwakuwa hali ya Orlando Pirates imegeukia upande moja tu kwamba lazima wafanye tendo gumu la kufunga kwanza, basi Simba akapambane kutokuruhusu goli la ugenini.

Kwa mujibu wa tafiti hakuna mchezaji aliyekufa uwanjani kwa ajili ya kukaba hivyo Simba ndiyo ikawe silaha ya’ kukaba hadi kivuli’.

Cris Mugalu akimiliki mpira mbele ya wachezaji wa Orlando Pirates.

Simba inahitaji sare ya aina yoyote ile ama ifingwe bao moja bila ili mchezo uongezwe dakika 30 au mpaka wafike kwenye hatua ya kipigiana penati.

Hadi hapa nawapa Simba 51% kufuzu na wenyeji 49 % nikiamini zaidi kwenye kilichopo mkononi.

Sambaza....