Ligi

SIMBA itafungwa na hawa wachezaji wa YANGA

Sambaza....

Kesho Tanzania inasimama kwa dakika 90 Kila hisia zitakuwa Chang’ombe , sehemu ambayo inamiliki uwanja wa Taifa , uwanja ambao utaandaa mechi kati ya Simba na Yanga , mechi kubwa Afrika Mashariki na Kati. Simba inaingia ikiwa inaizidi Yanga alama 10, Simba ina alama 34 na Yanga ina alama 24. Wafuatao ni baadhi ya wachezaji wa YANGA wanaoweza kuleta madhara kesho kwa Yanga.

PAPY TSHISHIMBI

Huyu ashawahi kusema mwenyewe kwenye mechi kubwa kama za Simba na Yanga huwa anacheza mpaka kiwango chake cha mwisho . Na kwa kweli huwa anafanya hivo , mechi nyingi za Simba na Yanga mmoja wa wachezaji ambao huwa wanang’ara sana ni Papy Kabamba Tshishimbi na kesho ana nafasi kubwa ya yeye kung’was kwenye mechi hii.

DEUS KASEKE

Mechi za hivi karibuni kiwango chake kimekuwa kikubwa sana , kasi yake ni silaha muhimu sana , kasi ambayo amekuwa akiitumia kutengeneza nafasi nyingi za magoli akiwa uwanjani. Mwezi Wa kwanza umemkuta akiwa bado yuko kwenye kiwango kizuri na Yanga wanahitaji mchezaji mwenye kasi kwa ajili ya mashambulizi ya kushtukiza kwa hiyo ni mmoja ya wachezaji ambao watakuwa na nafasi kubwa ya kuiangamiza Yanga kwenye mashambulizi ya kushtukiza.

 

PAPY SIBOMONA

Moja ya wachezaji hatari kwa sasa ni huyu , kuanzia mwezi wa kumi na moja mpaka mwezi wa kumi na mbili amefunga magoli 4 na kutoa pasi mbili za magoli amekuwa kwenye kiwango kizuri, chini ya Boniface Mkwasa amekuwa akicheza kama mchezaji huru na hii imempa nafasi ya yeye kuwa hatari zaidi na huyu atakuwa mchezaji hatari zaidi kwa Simba hiyo kesho.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.